Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TANZANIA KUANDAA MATAIFA AFRIKA MWAKA 2017

Tanzania imeomba kuandaa Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017, baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuiondoa Libya, iliyokuwa imepangwa kuwa mwenyeji wa michuano hiyo.

CAF ilitangaza kuiondoa Libya kutokana na kukumbwa na machafuko ya kisiasa nchini humo yaliyosababisha kutokuwa na serikali imara.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa (TFF), Selestine Mwesigwa, alisema wametumia nafasi hiyo kuomba kuwa wenyeji wa Afcon 2017.

Mwesigwa alisema uamuzi huo ulifikiwa na kupitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF,  iliyokutana juzi Dar es Salaam kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali.

Katibu huyo alisema tayari wamewasiliana na serikali na walitarajia kutuma maombi hayo jana CAF na kwamba wana imani kubwa  ya kukubaliwa,  kutokana na kuwa na sifa za kuandaa fainali hizo.

Alisema miundombinu walionayo inatosha wao kuandaa fainali hizo, hasa ikingizatiwa uwapo wa usalama wa kutosha hapa nchini.Endapo Tanzania itapata nafasi hiyo ya kuandaa michuano ya Afcon, itafuzu moja kwa moja kushiriki kinyang'anyiro hicho kwa sifa ya kuwa timu mwenyeji.

Hiyo itakuwa mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo katika historia yake kwani mara mwisho kucheza fainali hizo ilikuwa 1980 wakati huo ikinolewa na Joel Bendera ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, huku nahodha akiwa ni Rais Mstaafu wa TFF, Leodegar Tenga.

Katika hatua nyingine, Mwesigwa alisema katika kupinga upangaji wa matokeo kwenye mechi mbalimbali za mashindano, endapo akibainika mtu kufanya kitendo hicho atafungiwa maisha kutojihusisha na masuala ya soka.

Kadhalika Mwesigwa alisema Kamati ya Utendaji ya TFF, imemteua Boniface Wambura kuwa Mkurugenzi wa Mashindano  wa shirikisho hilo, kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu.

Mwesigwa alisema nafasi aliyokuwa nayo ya Ofisa Habari na Mawasiliano ipo wazi na wametangaza ajira mpya kwa nafasi hiyo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa