'WAASI WA M23' WAIBUKIA SHEREHE DAR.
Hali si shwari hasa kwa wakazi wa maeneo ya Tabata na Kigogo jijini Dar es Salaam kufuatia kutokea kwa kikundi cha vijana wadogo wenye umri wa miaka 12-17 wanaojiita 'Waasi wa M23' kuvamia sherehe mbalimbali na kufanya vurugu huku wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, visu na bisibisi. Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Mambo Uwanjani Leo ambao huko jirani na maeneo hayo umebaini kuwa kikundi cha vijana hao wanajitokeza nyakati za usiku kwenye sherehe za aina mbalimbali zinazohusisha muziki.