JEURI YA PESA, RAIS REAL MADRID KUVUNJA REKODI NYINGINE YA USAJILI ULAYA

RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez amesema kwamba mapato ya klabu yake tajiri zaidi duniani yanaweza kumnunua mshambuliaji wa Monaco, raia Colombia, Radamel Falcao mwakani.


Akizungumza katika chati ya shoo ya soka, Punto Pelota jana usiku, Perez alitolea nje uwezekano wa usajili wa Falcao katika dirisha dogo Januari, lakini akasema Real lazima iwe karibu naye mwishoni mwa msimu.

Falcao, mwenye umri wa miaka 27, aliondoka kwa wapinzani wa Jiji wa Real, Atletico kwenda kujiunga na Monaco mwishoni mwa msimu uliopita kwa dau lililoripotiwa kuwa kiasi cha Pauni Milioni 53.

"Yeye (Falcao) hatakuja Januari, lakini Juni, nani anafahamu?"alihoji Perez. "Hakuna kisichowezekana na kuna muda wa kutosha kutoka sasa hadi huko.

"Falcao ni mchezaji mkubwa na ninajua anataka kucheza (Real) Madrid. Ninatambua hilo, lakini ni kawaida. Wameniambia,".

Sababu moja kubwa Real kuingia sokoni kusaka mshambuliaji ni kushuka kwa kiwango cha mshambuliaji wake Mfaransa, Karim Benzema.

Kipenzi hicho cha Perez, Benzema ameshindwa kuteka hisia za mashabiki wa Real tangu awasili mwaka 2009 na hana furaha sana mbele ya umati wa Bernabeu.

Perez amekuwa akimtetea mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye amekuwa akilaumiwa na kocha wa Real, Carlo Ancelotti kwa kutojituma kiasi cha kutosha uwanjani.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA