LEWANDOWSKI ATUA BAYERN MUNICH
MSHAMBULIAJI Robert Lewandowski atapokea dau la usajili la karibu Pauni Milioni 10 atakapojiunga na Bayern Munich kama mchezaji huru mwishoni mwa msimu.
Mabosi wa Allianz Arena wamepuuzia madai kwamba mshambuliaji huyo wa Borussia Dortmund ana fikra mbadala juu ya kujiunga na Bayern na wamesistiza watamalizana naye wakati wa mwaka mpya.
Haruhusiwi kuingia kwenye mazungumzo rasmi na timu yoyote hadi wakati huo, ambazo zimefanikisha makubaliano ya Mkataba wa miaka minne, ambao yeye atapewa dau la kumwaga wino la Pauni Milioni 9 na mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki.
Uthibitisho wa kuhamia kwake Bayern ni pigo kwa klabu za Manchester United na Chelsea, ambao walikuwa na matumaini ya kumnasa na kuwapiku mabingwa wa Bundesliga, kufuatia maelezo yake wakati wa maandalizi ya mchezo wa timu yake ya taifa, Poland dhidi ya England uliopigwa Uwanja wa Wembley Jumatano usiku.
Alipoulizwa kuhusu mustakabali wake, alisema: "Nitakuwa tayari kusaini Mkataba na klabu yoyote Januari, lakini sijawahi kusema nitasaini Mkataba na Bayern. Siku moja, ningependa kucheza Ligi Kuu (England). Itakuwa uzoefu babu kubwa,".