KIBADENI AWEKWA NJIA PANDA SIMBA.......YADAIWA ANAWAGAWA WACHEZAJI

Uongozi wa Simba umetupilia mbali madai ya kocha wao, Abdallah Kibadeni aliyewatuhumu baadhi ya wachezaji wake kuihujumu timu hiyo katika mchezo dhidi ya Yanga uliofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Baada ya mechi hiyo iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3, Kibadeni aliwashushia lawama baadhi ya wachezaji wake kwamba waliihujumu timu hiyo kwa kucheza chini ya kiwango.

Kutokana na hali hiyo Makamu Mwenyekiti wa Simba, Joseph Itang’are alisema mambo hayo hayana nafasi kwa sasa wanachoangalia ni mechi zao zilizobakia katika mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.

Alisema baada ya mechi hizo ndipo watakapokaa na kufanyia  kazi shutuma hizo, lakini kwa sasa hawana nafasi hiyo.


“Mambo hayo naomba tuyaache kwa sababu hivi sasa akili zetu zipo juu ya mechi zetu za mzunguko wa kwanza zilizobakia dhidi ya Coastal Union, Azam  na Kagera Sugar ambazo tunatakiwa kushinda ili tujiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA