LEWANDOWSKI AISAMBARATISHA ARSENAL

BAO la dakika za lala salama la Robert Lewandowski limeipa ushindi wa 2-1 Borussia Dortmund dhidi ya Arsenal katika Ligi ya Mabingwa Uwanja wa Emirates usiku huu.

Henrikh Mkhitaryan aliifungia bao la kuongoza Borussia Dortmund, lakini Olivier Giroud akasawazisha ikawa 1-1.

Lakini katika dakika 10 za mwisho, Arsenal ikatepeta na kumruhusu mshambuliaji Lewandowski kuwamaliza nyumbani.


Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Ramsey, Arteta, Wilshere, Ozil, Rosicky na Giroud.

Borussia Dortmund: Weidenfeller, Grosskreutz, Subotic, Hummels, Schmelzer, Bender, Sahin, Blaszczykowski, Mkhitaryan, Reus na Lewandowski.

Katika mchezo mwingine, Chelsea imeshinda ugenini mabao 3-0 dhidi ya Schalke yaUjerumani, mabao ya Fernando Torres mawili na Eden Hazard moja.
Nayo AC Milan imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani na Barcelona katika mechi ya Ligi ya Mabingwa usiku huu Uwanja wa San Siro.

Robinho alitangulia kuwafungia wenyeji bao dakika ya tisa, pasi ya Mbrazil mwenzake, Kaka- lakini Lionel Messi akaisawazishia Barca dakika ya 24 kwa pasi ya Iniesta.

Mechi nyingine, Steaua Bucuresti imetoka 1 - 1 na
Basel, Olympique Marseille imefungwa 2-1 na Napoli, Porto imelala 1-0 mbele ya Zenit, Austria Wien imefungwa 3-0 na Atletico Madrid    na Celtic imeshinda 2 - 1 dhidi ya Ajax.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA