MAN CITY, MAN UNITED, CHELSEA JINO KWA JINO CAPITAL ONE.

KLABU ya Tottenham itamenyana na West Ham katika Robo Fainali za Kombe la Ligi, maarufu kama Capital One wakitakiwa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 3-0 katika Ligi Kuu  mwezi huu.

Spurs ilipigana na kutoka nyuma kwa mabao 2-1 katika dakika za nyongeza na kuipiga Hull Jumatano mabao 8-7 kwa mikwaju ya penalti.

Katika mechi nyingine za hatua hiyo ya michuano hiyo, Manchester United itasafiri hadi Stoke wakati Manchester City itamenyana na Leicester.


Timu ya Jose Mourinho, Chelsea iliyoitoa Arsenal kwa mabao 2-0 Jumanne itamenyana na Sunderland au Southampton.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA