'WAASI WA M23' WAIBUKIA SHEREHE DAR.
Hali si shwari hasa kwa wakazi wa maeneo ya Tabata na Kigogo jijini Dar es Salaam kufuatia kutokea kwa kikundi cha vijana wadogo wenye umri wa miaka 12-17 wanaojiita 'Waasi wa M23' kuvamia sherehe mbalimbali na kufanya vurugu huku wakiwa na silaha za jadi yakiwemo mapanga, visu na bisibisi.
Kwa mujibu wa uchunguzi uliofanywa na mtandao wa Mambo Uwanjani Leo ambao huko jirani na maeneo hayo umebaini kuwa kikundi cha vijana hao wanajitokeza nyakati za usiku kwenye sherehe za aina mbalimbali zinazohusisha muziki.
Vijana hao hufanya vurugu na uparaji ambapo mamia ya watu wamekuwa wakilalamika kuporwa mali zao ikiwemo simu na fedha, waathilika wakubwa ni akina mama ambao wamekuwa wahuzuliaji wakubwa katika sherehe hizo ambapo wameweza kulizwa na vijana hao.
Tayari vijana hao wameshafanya uasi wao na kuendelea kuwa tishio kwa wakazi waishio maeneo hayo na mengineyo jirani, kikundi hicho kilichokusanya vijana wenye kuhitajika na taifa kwa ajili ya masomo wamejikuta wakijiingiza kwenye uharifu huo, pia wanatumia dawa za kulevya ikiwemo bangi na mirungi.
Baadhi ya wakazi wa Tabata na Kigogo wamefanikiwa kuzungumxa na mtandao kwa kukata kutaja majina yao wamedai kuwa kikundi hicho ni hatari kwao kwani hutumia silaha za jadi na kuzuru watu, mbali zaidi jeshi la polisi limeshindwa kuwathibiti vijana hao hasa kutokana na kutofahamika vizuri.
Mkazi mwingine wa Tabata amelitaka jeshi la polisi kujitokeza mara wanapoombwa ili kuweza kuwabaini waharifu hao wanaochafua sura ya jiji la Dar es Salaam na nchi kwa ujumla, 'Kwanza wanajiita Waasi wa M23' ambao ni hatari kwetu' alisema mkazi mmoja wa Kigogo.
Kuwepo kwa kikundi hicho kunarudisha enzi za vikundi vya Komando Yosso na Kiboko ya Msheli vilivyokuwa tishio kwa wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake.