KIBADENI APEWA MECHI MBILI KABLA YA KUTIMULIWA.

Kuna taarifa zimeenea ambapo Mambo Uwanjani Leo imezipata kwamba kocha mkuu wa Simba SC Abdallah Kibadeni, amepewa mechi mbili za mwisho kabla ya kutimuliwa na uongozi wa timu hiyo baada ya kushindwa kuifikisha Simba kwenye kilele cha mafanikio.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi ambacho ni rafiki wa karibu na klabu ya Simba kinasema kuwa uongozi wa Simba umechoshwa na hali iliyopo kwa sasa katika klabu hiyo ambapo nidhamu ya wachezaji imeshuka mno.

Uongozi huo unadai ni tofauti kubwa kati ya Simba inayonolewa na Kibadeni na ile iliyokuwa ikinolewa na Mfaransa Patrick Liewig ambayo ilionekana kuwa na nidhamu ya hali ya juu iliyopelekea kukamata nafasi ya tatu ya msimamo wa ligi msimu uliopita.

Chanzo hicho kinadai kuwa Simba kwa sasa imepoteza mwelekeo na lawama zota anabebeshwa Kibadeni ambaye ndiye kocha mkuu, chanzo hicho kinaongeza kuwa Kibadeni ameshindwa kusimamia nidhamu ya wachezaji iliyowapelekea kucheza chini ya kiwango katika mechi zake mbili dhidi ya Coastal Union ambapo zilitoka suluhu ya 0-0 kisha na Azam ambapo Simba ililala 2-1.


Kuna uwezekano mkubwa mikoba ya Kibadeni akapewa kocha wa kikosi cha pili Simba B Seleman Matola ambaye anapigiwa chapuo na baadhi ya wanachama wa timu hiyo, uwezekano mkubwa Matola kupewa timu kutokana na ukaribu wake na wachezaji wa Simba wengi wao ni vijana waliokuwa chini yake

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA