HAMISI KIIZA AMGWAYA TAMBWE, UFUNGAJI BORA

Mshambuliaji  Mganda Hamis Kiiza wa Yanga amesema kuwa kwa sasa hawazii kiatu cha dhahabu cha mfungaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, bali mawazo yake yamejikita katika kuhakikisha anaisaidia timu yake kutetea ubingwa wa ligi hiyo.

Kiiza alisema baada ya mazoezi ya Yanga kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola uliopo Mabibo jijini Dar es Salaam jana kuwa hashindani na wachezaji wengine kusaka zawadi ya mfungaji bora bali anasaka mafanikio ya kikosi cha 'Wanajangwani'.


"Kikubwa ni kutetea ubingwa, zawadi ya mfungaji bora siifikirii sana kwa sasa. Naamini kufunga magoli mengi kutaisaidia timu yetu kuibuka bingwa tena. Na tukishakuwa na magoli mengi, kiatu cha dhababu kitakuja chenyewe, alisema Kiiza ambaye juzi alifunga goli moja na kufikisha magoli nane katika michezo saba ya ligi hiyo msimu huu.
Amemfikia aliyekuwa kinara pekee, Amisi Tambwe wa Simba.

Katika hatua nyingine, kiungo 'fundi' Haruna Niyonzima 'Fabregas' , aliyeukosa mchezo wa juzi walioshinda 3-0 dhidi ya Mgambo JKT kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutokana na matatizo ya kifamilia, anatarajiwa kurejea mazoezini leo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kizuguto, kiungo huyo atarejea dimbani leo kujiandaa kwa mchezo wao wa kesho dhidi ya JKT Ruvu ya Pwani utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa baada ya kumalizika kwa siku tatu za ruhusa aliyoomba kwa ajili ya kumaliza matatizo ya kifamilia yaliyokuwa yanamkabili.

Niyonzima alirejea kwao Rwanda siku nne zilizopita na alitarajiwa kurudi jana kuungana na kikosi cha kocha Mholanzi Ernie Brandts.

Wachezaji wengine wa Yanga ambao walikosa mazoezi ya jana yaliyofanyika kwa saa mbili kuanzia saa 3:00 asubuhi kutokana na majeraha ni pamoja na kiungo Nizar Khalfan, beki wa pembeni Juma Abdul na kiungo Salum Telela.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA