YANGA YAZITEGA SIMBA, AZAM NA MBEYA CITY

Unaweza kushangaa lakini ndivyo itakavyokuwa kuwa mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga inaweza kukamata usukani wa ligi kuu Tanzania bara inayoelekea ukingoni endapo tu vinara wa ligi hiyo Simba, Azam na Mbeya City zitafanya makosa katika mechi zao za wao kwa wao.

Yanga kwa sasa iko katika nafasi ya nne na inaweza kukamata usukani wa ligi endapo itamaliza mechi zake za mwisho vizuri kwani inacheza na timu dhaifu, Lakini Simba Sc wiki ijayo inakutana na Azam FC kwenye uwanja wa Taifa ambapo kama timu hizo zitatoka sare nasi Yanga inaweza kuzivuka kirahisi.


Yanga itacheza na Mgambo Shooting timu ambayo ni dhaifu na inayoshika mkia, pia Mbeya City ambayo itakutana na Azam inaweza kuweka pengo lingine kwa Yanga endapo zitatoka sare ama mmoja kumfunga mwenzake, mwishoni mwa wiki hii Mbeya City itakutana na hasimu wake Prisons jijini Mbeya

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI