IVO MAPUNDA ACHEKELEA KUITWA STARS.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen alitangaza kumjumuisha kwa mara ya kwanza kipa Ivo Mapunda katika kikosi cha wachezaji 30 watakaoingia kambini kujiandaa na Michuano ya Chalenji itakayofanyika Nairobi, Kenya kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12.
Mapunda aliwahi kuwa kipa tegemeo wa Taifa Stars iliyokuwa chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo na kuisaidia kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) zilizofanyika Ivory Coast 2009.
Mapunda akizungumza na kwa simu kutoka Kenya alisema: “Nimesoma taarifa za kuitwa katika kikosi cha Kilimanjaro Stars leo asubuhi kupitia mitandao ya kijamii, hakika nilishtuka.
“Nimefurahi sana kuitwa kwa mara nyingine kuichezea nchi yangu, nasema ni fahari kubwa kwangu. Unajua kwa nini nilishtuka! Sikuwa na matarajio ya kuitwa tena, nilijua labda muda wangu umepita kumbe kocha anafuatilia kile tunachokifanya.”