KIBADENI AANZA VISINGIZIO, ADAI HAJAPATA FIRST ELEVEN......
Kocha Mkuu wa Simba, Abdallah Kibaden ameweka wazi kuwa bado hajapata kikosi cha kwanza na kudai amebakisha mechi mbili za majaribio ili kupata ‘first eleven’ yake ambapo mechi yao na Yanga Jumapili itakuwa miongoni mwa mechi hizo.
“Simba inahitaji kucheza mechi 10 ambazo zitaniongoza mimi kama kocha kuona nani anastahili kucheza kwenye ‘first eleven’ yangu,” alisema kocha huyo.
Kibaden alisema hivi sasa analazimika kumtumia kila mchezaji kwenye mechi za Ligi Kuu inayoendelea nchini ili kubaini kiwango cha kila mchezaji na kusisitiza kuwa kikosi chake cha kwanza kitajulikana baada ya kucheza michezo 10 ya Ligi Kuu.
Simba itashuka uwanjani Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza dhidi ya Yanga ikiwa ni mchezo wa tisa wa majaribio kwa kocha Kibadeni katika kuangalia uwezo wa wachezaji wake.
“Mechi yetu ya mwisho na Tanzania Prisons (Simba ilishinda 1-0) ndiyo ilikuwa mechi yangu ya nane katika kuwapima vijana wangu, nimebakisha mechi mbili za mwisho ambapo baada ya mechi hizo Simba itakuwa imekamilika kwa kuwa na kikosi cha kwanza,” alisema.
Mechi ya mwisho ya majaribio ya Simba itakuwa dhidi ya Coastal Union ya Tanga ambayo ni mechi ya 10 kwa kikosi hicho huku Kocha Kibaden akidai anahitaji kuwa na kikosi cha kwanza kitakachoitumikia Simba kwa dhati na si vinginevyo.
Hata hivyo hii siyo mara ya kwanza kwa kocha Kibaden kutoa kauli hiyo ya kutafuta kikosi chake cha kwanza kwani amekuwa akizungumza mara kwa mara kwamba baada ya kucheza mechi kumi za Ligi Kuu siyo mechi za kirafiki ndiyo atakuwa amepata kikosi chake cha kwanza kwani atakuwa amepata nafasi kubwa ya kuwasoma wachezaji wake wote, ambapo karibu kila mechi amekuwa akiwapa nafasi wachezaji tofauti.