MAGAIDI WAWILI WA 'WESTGATE' WAPATIKANA KENYA........

Miili miwili iliyoungua vibaya aliyoopolewa katika eneo la kituo cha biashara cha Westgate nchini Kenya siku ya Alhamisi inawezekana kwa kiasi kikubwa ikiwa ni ya magaidi walioshambulia kituo hicho, Mbunge mmoja wa Kenya ameiambia BBC.


Ndung'u Gethenji mwenyekiti wa kamati ya Bunge inayochunguza shambulio hilo pia amesema mwili mwingine ambao umepatikana unawezekana kwa kiasi kikubwa ukawa ni wa mmoja wa wanajeshi.

Mamlaka ya Kenya kwa sasa inaendelea na uchunguzi wa kisayansi wa miili hiyo.

Karibu watu wapatao 67 walifariki dunia wakati magaidi wanaodhaniwa kuwa ni wa kundi la wanamgambo wa Al Shaabab waliposhambulia kituo hicho Septemba 21 mwaka huu.

Shambulio hilo lilisababisha eneo hilo kuzingirwa kwa siku nne ambapo pia sehemu kubwa ya kituo hicho cha biashara iliharibiwa.

Mamlaka ya Kenya imeyataja majina manne ya watuhumiwa wa shambulio hilo, japo hawajatoa ufafanuzi zaidi.

Bado haijajulikana kama magaidi waliofanya shambilizi hilo kama walitoroka au la na pia imekuwa ni vigumu kujua idadi ya magaidi waliohusika kwenye tukio hilo.

Awali maafisa wa serikali ya Kenya walisema inakadiriwa magaidi hao walikuwa kati ya 10 na 15 lakini picha za CCTV zilionyesha magaidi wapatao wanne tu ndo waliokuwepo kwenye tukio hilo.

Tayari Kundi la Kigaidi la Al Shabaab limeshakiri kuwa ndilo lililohusika na shambulio hilo kufuatia majeshi ya Kenya kwenda nchini Somalia kupambana na kundi hilo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA