KAGERA SUGAR WAPANIA KUISHUSHA SIMBA NAFASI YA NNE
Wakati mshambuliaji mpya wa Simba Mrundi Amisi Tambwe akirejea uwanjani na kuanza mazoezi, uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umetamba kuwa timu yao itaendeleza ubabe dhidi ya 'Wanamsimbazi' kwa kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katika mechi ya mwisho baina ya timu hizo, Kagera Sugar iliyokuwa ikifundishwa na kocha wa sasa wa Simba, Abdallah Kibadeni, iliwafunga Wekundu wa Msimbazi 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba Machi 27, 2013 baada ya timu hizo kutoka sare ya 2-2 jijini Dar es Salaam Oktoba 17, 2012.
Akizungumza na jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Kagera Sugar, Hamis Madachi alisema kikosi chao kinachonolewa na kocha Mganda Jackson Mayanja, kimeandaliwa vizuri kwa ajili ya mchezo huo.
"Hatuna wasiwasi na timu yetu katika mchezo wa leo kwa sababu tunawaelewa vizuri Simba. Kikosi chetu kilitua Dar es Salaam juzi na jana kinaendelea na mazoezi maeneo ya Tandale kujiweka sawa kabla ya kuwakabili Simba," alisema Madachi na kuongeza:
"Mara nyingi timu za nje ya Dar es Salaam zinapokuja kucheza kwenye Uwanja wa Taifa zinakuwa na hofu lakini sisi hatuna cha kuogopa kwenye Uwanja wa Taifa. Tutaendeleza kipigo kwa Simba leo."
Katika hatua nyingine, mshambuliaji Mrundi Amisi Tambwe wa Simba aliyekosa mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara waliyolala 2-1 dhidi ya Azam Jumatatu kutokana na maumivu ya goti, jana alianza mazoezi mepesi kujiandaa kuwakabili Kagera Sugar.
Daktari wa Simba, Yassin Gembe alisema jana kuwa Tambwe alifanya mazoezi mepesi jana asubuhi Bamba Beach, Kigamboni na alitarajiwa kufanya mazoezi jioni pia.
“Baada ya hapo tutaangalia hali yake kama ataweza kucheza kesho (leo) au la. Hatutamlazimisha kucheza kama hajapona sawa sawa, kwa sababu ni hatari kwake na kwa timu pia,” alisema Gembe.
Tambwe, alicheza dakika zote 810 katika mechi tisa za Simba akianza na mchezo wao wa pili msimu huu dhidi ya Oljoro JKT jijini Arusha Agosti 28 akihitimisha katika mchezo wake wa tisa waliotoka suluhu dhidi ya Coastal Union jijini Tanga Oktoba 23.
Simba itarejea kileleni kama itashinda mechi ya leo kwa kuwa itafikisha pointi 23, sawa na vinara Azam na wageni wa ligi hiyo Mbeya City walio katika nafasi ya pili kwa sasa. Tofauti nzuri ya magoli itawabeba Simba.
Yanga, waliopata ushindi wa 3-0 dhidi ya timu ya mkiani mwa msimamo, Mgambo JKT juzi, watashuka kwenye Uwanja wa Taifa kesho kuwakaribisha 'maafande' wa JKT Ruvu katika mechi nyingine ya ligi hiyo.
Keshokutwa kutakuwa na mechi nne; Mgambo Shooting na Coastal Union (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga), Prisons na Oljoro JKT (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Azam na Ruvu Shooting (Azam Complex, Dar es Salaam) na Mtibwa Sugar na Rhino Rangers (Uwanja wa Manungu, Morogoro).
Raundi ya 12 ya ligi hiyo inayoshirikisha timu 14, itakamilika Jumapili kwa mechi moja, Mbeya City itapokuwa mwenyeji wa Ashanti United kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashani United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, Rhino Rangers vs Tanzania Prisons na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7, Azam itacheza dhidi ya Mbeya City (Azam Complex, Dar es Salaam) wakati Yanga itacheza dhidi ya Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam