MAN CITY WAWASIRI URUSI BILA NAHODHA WAO
Kikosi cha Manuel Pellegrini kitamenyana na jkabu ya Urusi wiki hii, kikitarajia kuzinduka baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Bayern Munich katika mchezo uliopita.
Lakini Kompany, sambamba na Martin Demichellis na Jack Rodwell, hawajasafiri na timu.
Beki mshirika wa kudumu Kompany pale katikati Matija Nastasic alianza pamoja na Javi Garcia, ambaye kwa kawaida hucheza kama kiungo mkabaji.Kompany alirejea uwanjani wiki za karibuni baada ya kukosa mechi kibao za mwanzo wa msimu, lakini akaumia tena na kukosa mechi ya Jumamosi timu hiyo ikishinda dhidi ya West Ham.
City iliifunga Everton 3-1 kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa, na Pellegrini akabadilisha akabdilisha mabeki wake wanne katika ushindi wa Jumosi Upton Park, kwa Joleon Lescott, Kompany, Pablo Zabaleta na Aleksandar Kolarov wakichukua nafasi za Nastasic, Garcia, Micah Richards na Gael Clichy.
Pamoja na hayo, City iliruhusu nyavu zake kutikiswa mwishoni mwa wiki, Garcia - ambaye alichezeshwa nafasi isiyo yake, alionekana kucheza kwa uelewano mkubwa na Nastasic.
Sergio Aguero, aliyefunga mabao mawili katika ushindi wa West Ham, alikuwa vizuri, sambamba na Joe Hart na Yaya Toure.