Tuzo ya MVP yamponyoka Feitoto


Inawezekana ubora wa Feisal Salum Feitoto' usitoshe pekee kumbeba kwenye mbio za tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP) ikiwa hana ubingwa wa Ligi Kuu mkononi.

Mambo yamebadilika kwenye takwimu:
Asisti: Elie Mpanzu sasa ndiye kinara akiwa nazo 9, akimwacha Fei Toto mwenye 8.

Ufungaji: Yupo sawa na Mossi Ndumumwe, wote wakiwa na mabao 14, Allan Okello hayupo mbali (11).

Bila kombe la Ligi Kuu, njia pekee ya Fei kutwaa tuzo ya MVP inakuwa ni kutawala takwimu zote mbili.

Mchezo wa jana dhidi ya Yanga SC unaweza ukawa umehamisha mjadala mzima kwenda kwa wachezaji wa Simba au Yanga (iwapo mmoja wapo akibeba ubingwa), labda tu kama Feisal atarejesha ufalme wake kileleni kwenye takwimu.

Haina ubishi, Fei Toto ni kiungo mfungaji bora zaidi nchini tangu atue Chamazi, lakini mechi dhidi ya Coastal Union na Dodoma Jiji ndizo zitakazoamua hatma yake.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI