Barker aeleza mambo matano kuelekea mechi ya kesho

Mambo 5 Aliyoyasema Kocha Steve Barker Kuelekea Mechi ya Kesho Dhidi ya Singida Black Stars: (LIGI KUU).

Tahadhari kwa Mossi Ndumumwe: Barker amekiri kuwa safu ya ushambuliaji ya SBS ni hatari, na Kinarabwa mabao Mossi Ndumumwe amekuwa na moto mkali tangu Januari. Ni mtu wa kuchungwa kwa ukaribu sana.

Matumaini ya Ubingwa: Simba bado hawajakata tamaa. Hesabu ni kushinda mechi zao zote huku wakivizia wapinzani wao kuteleza na kudondosha pointi.

Vita ya Mbinu: Kocha anaamini wachezaji wake wamekomaa zaidi kimbinu kuliko wapinzani wao, hivyo ushindi kesho ni amri!

Ripoti ya Kikosi: Kibabage bado yuko mashakani kuanza hali yake (itaendelea kuangaliwa leo), Anicet Oura kuna uwezekano mkubwa akaanza, na habari njema ni kurejea kwa Morice Abraham kutoka majeraha.

Nguvu ya Mashabiki: Barker amewapongeza Wanasimba kwa support ya maana tangu ameanza kazi Msimbazi, na anaomba mzigo uendelee kesho.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI