Seleman Mwalimu atabaki Simba
Kocha Steve Barker amemtaja Selemani Mwalimu kuwa mmoja wa washambuliaji anaotaka kubaki nao Simba SC kuelekea msimu wa 2026/27
Mkataba wa sasa wa mkopo wa Selemani Mwalimu na Simba SC hauna kipengele chochote cha kuongeza muda wa mkopo au kumnunua moja kwa moja
Hii ina maana kuwa Mwalimu anatakiwa kurejea Wydad AC mara baada ya mkopo wake kumalizika, then Simba SC na Wydad AC wafungue mazungumzo mapya(kama wanahitaji kubaki naye)
Taarifa zinaeleza kuwa Wydad AC wako tayari kumruhusu Mwalimu aondoke kwa uhamisho wa moja kwa moja(kuuzwa), na si kwa mkopo mwingine
Hata hivyo, ada inayotarajiwa kuhitajika inaweza kuwa changamoto kwa Simba SC
Licha ya kuvutiwa na vilabu kadhaa, Selemani Mwalimu ameipa Simba SC kipaumbele na yuko tayari kusubiri uamuzi wa Simba sc kabla ya kusikiliza ofa nyingine
Kwa sasa, mchezaji anaitaka Simba kwanza... lakini uamuzi wa mwisho utategemea kama Simba SC na Wydad AC watafikiana
