Azam FC yamkomalia Iddi Nado kwenda Yanga
Azam FC imeanza mazungumzo na kiungo wake Nado kwa lengo la kuongeza mkataba wake, kufuatia kiwango bora alichoonyesha tangu aliporejea kikosini mwezi Julai 2025.
Nado, ambaye alijiunga na Azam FC mwaka 2019 akitokea Mbeya City, ameendelea kuwa mmoja wa wachezaji muhimu ndani ya kikosi hicho kutokana na mchango wake mkubwa katika safu ya kiungo.
Taarifa zinaeleza kuwa hatua ya Azam FC kumuita mezani inalenga kuhakikisha inamdumisha nyota huyo, hasa baada ya kuvutia macho ya watani wa jadi, Yanga SC na Simba SC, ambao wanatajwa kuwa na nia ya kupata saini yake.
Hatma ya Nado sasa inategemewa kuamuliwa na mazungumzo kati yake na Azam FC huku dirisha la usajili likiendelea kushika kasi.
