Yanga yaikandika Azam FC 3-0

MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara nuliofanyika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar jioni ya leo.

Mabao ya Yanga yamefunwa na beki Ibrahim Hamad Abdullah ‘Bacca’ dakika ya 41, mshambuliaji Laurindo Dilson Maria AurĂ©lio ‘Depu’ kutoka Angola dakika ya 73 na kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 81.

Kwa ushindi huo, Yanga SC wanafikisha pointi 69 na kuendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi mbili ya watani wao, Simba baada ya timu hizo zote kucheza mechi 28 kuelekea mechi mbili za kukamilisha

Kwa upande wao Azam FC baada ya kupoteza mchezo huo wanabaki na pointi zao 58 wakibaki pia katika nafasi ya tatu mbele ya Singida Black Stars yenye pointi 50 kufuatia timu hizo nazo kucheza mechi 28.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI