Diarra kinara wa clean sheets
Kipa wa Yanga SC na Timu ya Taifa ya Mali, Djigui Diarra, ameendelea kuonyesha kiwango cha juu baada ya kufikisha clean sheets 17 kufuatia mchezo dhidi ya TRA.
Rekodi hiyo inamfanya kuwa kipa mwenye clean sheets nyingi zaidi msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku kukiwa bado kumesalia mchezo mmoja kabla ya msimu kumalizika.
Hii ni mara ya tatu kwa Djigui Diarra kumaliza akiwa kinara wa clean sheets tangu ajiunge na Yanga SC, jambo linaloonyesha uthabiti wake langoni kwa misimu kadhaa mfululizo.
Rekodi zake za Clean Sheets:
2021/22 – 15
2022/23 – 17
2023/24 – Ley Matampi (15)
2024/25 – Moussa Camara (19) 2025/26 – 17 (bado mchezo mmoja umebaki)
Djigui sasa ana nafasi ya kuongeza idadi hiyo katika mchezo wa mwisho wa msimu na kuendelea kuimarisha rekodi yake kama mmoja wa makipa bora kuwahi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara.
