Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2016

Simione Zaza akataliwa West Ham

Picha
Wakala wa mshambuliaji wa Juventus, Simione Zaza anayekipiga kwa mkopo West Ham, Vincenza Morabito amesema nyota huyo ataondoka West Ham katika dirisha la usajili la January kurejea klabuni kwake Juve. Zaza alitua West Ham majira ya joto lakini hajafanya la maana kwani katika mechi 10 za timu hiyo alizocheza kwenye Primier na kombe la EFL hajaifungia bao lolote. "Zaza kwa vyovyote anarudi Juve kwa sababu West Ham hawamtaki kwa sasa", alisema Morabito ambaye ni wakala wa straika huyo anayekumbukwa kwa kuweka mbwembwe nyingi kwenye oenalti kisha akakosa katika Robo fainali ya Euro 2016 dhidi ya Ujerumani hali iliyoigharimu Italia kufungasha virago

Taifa Jang' ombe yaifanyizia Jang' ombe Boys

Picha
Na Prince Hoza, Zanzibar Timu ya Taifa Jang' ombe maarufu Wakombozi wa Ng' ambo usiku wa leo wameibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Amaan Zanzibar mchezo wa ufunguzi kombe la Mapinduzi. Ushindi huo umewapa nguvu Wakombozi hao wa Ng' ambo ambao Jumapili watacheza na Wekundu wa Msimbazi usiku wa saa 2:30 uwanja huo huo wa Amaan. Michuano hiyo itaendelea tena Jumapili ya January mosi mwaka 2017 ambapo jioni ya saa 10: 00 KVZ na URA zitaumana na kufuatiwa na mchezo mwingine utakaopigwa usiku wa saa 2:30 Simba SC itakapocheza na Taifa Jang' ombe

Kipute Mapinduzi Cup kuanza leo, watani kufungua dimba

Picha
Na Prince Hoza, Zanzibar Michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza leo katika uwanja wa Amaan Zanzibar, mchezo wa ufunguzi utapigwa usiku saa 2:00 kati ya watani wa jadi Taifa Jang' ombe na ndugu zao Jang' ombe Boys. Wakati leo ukifanyika ufunguzi, kesho kutwa tarehe 1 January 2017 kutapigwa mechi mbili, jioni saa 10:00 KVZ ya Zanzibar itachuana na mabingwa watetezi URA ya Uganda na kufuatiwa na mchezo mwingine kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba SC na Taifa Jang' ombe

Valencia bado yamng' ang' ania Rojo

Picha
Valencia bado inakomaa kuhakikisha inamnasa beki wa Manchester United Marcos Rojo kwenye usajili wa dirisha dogo la January. Muargentina huyo ameanza kuaminiwa na Jose Mourinho lakini Valencia inaamini kutua kwa Victor Landelof kutamfanya Rojo awe huru na watampata kirahisi

Simba haikamatiki kileleni, yaizaba Ruvu Shooting 1-0

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Simba SC imezidi kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars baada ya jioni ya leo kuichapa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani bao 1-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi nne na mshindani wake mkuu Yanga iliyo katika nafasi ya pili, Simba sasa ina pointi 44 wakati Yanga wana pointi 40. Bao lililoipa Simba ushindi liliwekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Mohamed Ibrahim "Kabae", huo ni mchezo wa mwisho kwa mwaka huu kwani michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza kesho.

Juventus yamuwinda Kroos wa Real Madrid

Picha
Kule nchini Italia, Klabu ya Juventus ya Turin bado wanaendelea na mawindo yao ya kumnasa kiungo wa Real Madrid, Toni Kroos na wapo tayari kutoa hata Euro milioni 60 kwa ajili ya kiungo huyo Mjerumanj. Na kama Real Madrjd itakataa kumuuza kiungo huyo kwa Juve, wataelekeza nguvu zao kwa Marco Verratti wa PSG au Ivan Rakitic wa Barcelona

Azam yafukuza benchi la ufundi

Picha
Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam Uongozi wa Azam FC umelitimua benchi lake la ufundi hasa kufuatia mwenendo mbaya wa kikosi hicho, Kocha mkuu Mhispania Zeben Hernandez na msaidizi wake Jonas Garcia. Inadaiwa makocha hao wameshindwa kuiletea mabadiliko timu na ndio kwanza wameshusha morali, Azam haipo kwenye ushindani na miamba Simba na Yanga zinazofukuzana kileleni. Mpaka sasa Azam inasuasua ikishika nafasi ya tatu huku ikitoka sare mechi mbilj mfululizo na kuzidi kuongeza gepu la pointi na vinara wa Ligi hiyo Simba pamoja na Yanga wanaoshika nafasi ya pili. Kally Ongala ambaye kwa sasa ni kocha wa Majimaji ya Songea anatajwa kumrithi Mhispania huyo aliyekuja kwa mikwara akidai Paskal Wawa si beki na kuamua kuachana naye pamoja na kiungo Jean-Bapstita Mugilaneza akidai si kiungo

Yanga wanatupia tu, waichinja Ndanda 4-0

Picha
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam Mabingwa watetezi Yanga SC jioni ya leo imeichapa bila huruma.Ndanda FC mabao 4-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara. Mapema kabisa Yanga waliandika bao la kwanza na la pili yote takifungwa na mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ndombo Ngoma, Mrundi Amissi Joselyin Tambwe akaiandikia Yanga bao la tatu hivyo hadi mapumziko Yanga ilikuwa mbele. Kipindi cha pilj kilianza kwa kasi lakini Ndanda walionekana kubadilika na kucheza kwa taadhali kubwa ili wasifungwe odadi kubwa ya mabao, Beki Mtogo Vincent Bossou alifunga goli la nne na la ushindi ambalo liliwafanya Yanga wafikishe pointi 40 wakiendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya Simba inayoongoza Ligi. Mchezo mwingine Mtibwa Sugar imeifunga Majimaji ya Songea bao 1-0 katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro

Griezman aitosa Man United, sasa kutimkia Marekani

Picha
Straika wa Atletico Madrid Antoine Griezman amefunguka kuhusu nia yake ya kutaka kucheza soka Marekani huku kukiwa na tetesi kuwa Manchester United imekusudia kumchukua katika usajili wa majira ya joto (Juni- Juni). Griezman anasema "Naipenda Marekani, nataka kuwa na tiketi za msimu mzima wa NBA na niwe nakwenda kuangalia kila mechi nikiwa na watoto wangu", amesema mshambuliaji huyo. "Najiona mwenyewe nikiwa huko, Bado sijajua ni jiji gani nitaishi, aliongeza Griezman ambaye ni mfungaji anayetegemewa katika kikosi cha Atletico Madrid

Yadaiwa Cheka alimkwepa Dulah Mbabe

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Inasemekana bondia wa ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka alimkwepa bondia mwenzake Abdallah Pazi maarufu Dulah Mbabe ambaye ilikuwa apambane naye Desemba 25 wakati wa sikukuu ya Krismasi. Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Cheka ambaye amekataa kutaja jina lake, amesema Cheka amemkimbia Dulah Mbabe kwani kwa sasa uwezo wake wa kupigana umeshuka hivyo kama angezichapa naye huenda angepigwa vibaya. Rafiki huyo amedai Cheka tangia alipopigwa na bondia wa India Vijenger Singh, amepoteza mwelekeo na angejikuta anapigwa vibaya na Dulah Mbabe, "Cheka angepigwa na Dulah, suala la kulipwa na promota halina ukweli ni visingizo tu kwani angeumbuliwa vibaya na ngumi, kwa sasa Dulah ndiye mfalme wa masumbwi ukweli ndio huo" amesema rafiki huyo wa Cheka

Jerry Muro aibuka na kuiomba radhi TFF

Picha
Na Ikram Khamees, Dar es Salaam Msemaji wa Yanga SC, aliyekifungoni Jerry Muro ameibuka na kuiomba radhi TFF ili imwachie huru na aendelee na majukumu yake ya usemaji ndani ya Klabu hiyo inayokamata nafasi ya pili. Muro amesema bila yeye Yanga inapwaya kwani hadi sasa Simba inaongoza Ligi hiyo ikiwa imeiacha Yanga kwa tofauti ya pointi 4 na mtani wake Yanga. Jerry Muro alifungiwa na TFF kutokana na kutoa lugha chafu na kebehi kwa Shirikisho hilo la mpira wa miguu hapa nchini, lakini Muro ameliangukia Shirikisho hilo na kuliomba radhi na kudai kama atasamehewa basi ndio utakuwa mwisho wa Simba kuchonga

Southmpton yataka Pauni Milioni 40 kumwachia beki wake

Picha
Kazi bado ngumu katika mchakato wa kuinasa saini ya mlinzi mahiri Virgii Van Djik na Klabu yake imepanga mezani dau la Pauni Milioni 40 kwa timu yoyote ambayo inamwania staa huyo wa kimataifa wa Uholanzi. Van Djik anafukuziwa na Liverpool, Chelsea na Manchester City huku pia timu yake ya Southmpton nayo ikitaka huduma yake kama kawaida

Siri zavuja Ajibu kutimkia Misri

Picha
Na Saida Salum, Dar es Salaam Siri zimevuja baada ya mshambuliaji Ibrahim Ajibu kutimkia nchini Misri kufanya majaribio katika Klabu ya Al Haras Hadood inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo. Udukuzi uliofanywa na Mambo Uwanjani umebaini kuwa mshambuliaji huyo mwenye mabao matatu ameenda kufanya majaribio katika timu hiyo ili acheze soka la kulipwa baada ya kuona uwezo wa kupata namba katika kikosi cha kwanza haupo. Ajibu alikuwa akiwekwa benchi jambo lililopelekea aombe ruhusa ya kwenda kufanya majaribio, uongozi wa Simba umemruhusu na tayari mchezaji Hugo ameshaondoka nchini

Arsenal yamwania Isco

Picha
Arsenal wamerudi tena vitani katika kumnyatia kiungo wa Real Madrid, Isco na wanataka kumnasa katika Dirisha la January. Baada ya kubaini kuwa kiungo huyo hana raha Klabuni hapo msimu huu kutokana na kukosa nafasi ya kutosha katika kikosi cha kwanza

Simba siyo Yanga, yaichapa JKT Ruvu 1-0 na kuzidi kupaa kileleni

Picha
Na Prince Hoza, Dar es Salaam Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba SC jioni ya leo imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. JKT Ruvu ilicheza kandanda safi muda wote na kuonekana kuizuia Simba isipate bao katika kipindi cha kwanza lakini walishindwa kufanya hivyo kwani Shiza Ramadhan Kichuya aliweza kuifungia Simba bao la ushindi. Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 41 na kuzidi kuziacha kwa mbali Yanga na Azam ambazo ziko katika nafasi ya pili na ya tatu, Simba sasa itacheza na Ruvu Shooting kabla haijaelekea Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup

Nyosso asaini Mbeya Warriors

Picha
Na Exipedito Mataruma, Mbeya Mchezaji wa zamani wa Ashanti United, Simba SC, Coastal Union na Mbeya City, Juma Said Nyoso amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Mbeya Warriors ya Mbeya inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara. Nyoso aliyewahi kufungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kwa miaka miwili akidaiwa kumtomasa makalioni mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco "Adebayor". Adhabu ya mchezaji huyo inamalizika msimu huu hivyo Nyoso amesaini kama mchezaji huru, Beki huyo amekuwa akijifua kivyake ili kujiweka fiti zaidi

Tambwe ainusuru Yanga kulala mbele ya Lyon

Picha
Na Ikram Khamees Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga SC raia wa Burundi, Amissi Joselyin Tambwe ameinusuru timu yake kulala mbele ya African Lyon katika uwanja wa Uhuru baada ya kufungana mabao 1-1. Kwa matokeo hayo Yanga imebaki katika nafasi yake ya pili ikiwa na pointi 37 baada ya leo kushindwa kukwea kileleni endapo ingechomoza na ushindi. Timu hizo zinaenda mapumziko zilikuwa hazijafungana, lakini kipindi cha pili Lyon ilijipatia bao la kuongoza lililofungwa na Ludovic Venance, Amissi Tambwe aliiokoa Yanga baada ya kusawazisha goli na kufanya matokeo kuwa sare

KESSY AIGHARIMU YANGA MAMILIONI YA SHILINGI

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Kitendo cha Klabu ya Young Africans kupeleka jina la mchezaji wa klabu nyingine CAF huku mchezaji huyo akiwa ndani ya mkataba na mwanachama mwingine wa TFF ni kosa kubwa kwa mujibu wa kanuni za ligi kifungu 69[5] ambalo linapaswa kupewa adhabu itakayopelekea wanachama wote kuheshimu nafasi ya TFF kwenye suala la usajili na sio kuanza kwenda CAF au kwingineko ili kulinda integrity ya soka la Tanzania. Klabu ya Young Africans inatozwa faini ya Sh 3,000,000 (Sh milioni tatu) kwa mujibu wa kanuni na fidia kwa klabu ya Simba ya Sh 50,000,000 (Shilingi milioni hamsini). Ofisa wa TTF aliyehusika ama kwa kushirikiana na Uongozi wa Klabu ya Young Africans au kwa kutochukua hatua stahiki kwa wakati apelekwe kwenye mamlaka yake ya nidhamu, yaani, Katibu Mkuu wa TFF ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa dhidi yake.

Straika huyu hatari anakuja Jangwani kumrithi Chirwa

Picha
Na Saida Salum Maisha ya Mzambia Obrey Chirwa yako shakani katika klabu ya yanga kufuatia ujio wa mzambia mwenzake winston kalengo anayekipiga FC Leopards ya Congo Blazavile. Kalengo ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa kuliko chirwa ambaye anatajwa kupelekwa kwa mkopo FC Platinum ya Zimbabwe. Chirwa aliyesajiliwa kwa mamilioni ya shilingi ameshindwa kuisaidia Yanga licha ya kufunga magoli matano, Yanga hadi sasa inashika nafasi ya pili ikiwa nyuma ya Simba

YANGA KUJIPIMA NA JKU KESHO UHURU

Picha
Na Prince Hoza Kikosi cha Yanga  jumamosi tar 10/12/2016 kitakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU  toka Zanzibar. Mchezo utafanyika uwanja wa Uhuru utaanza saa 10 kamili jioni. Kiingilio cha mchezo huo kitakuwa sh.5000/ kwa mzunguko na 10000/= kwa VIP. Tiketi za mchezo huu zitakua ni za electroniki kwa kadi za Selcom. Mchezo huu utatumika kumuaga kiungo Mbuyu Twite.

Rasmi Yanga yaachana na Mbuyu Twite

Picha
Na Mrisho Hassan Mabingwa wa kandanda Tanzania Bara, Yanga SC, imeachana rasmi na beki wake kiraka Mkongoman Mbuyu Twite ambaye sasa ni mchezaji huru. Taarifa iliyotolewa na Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdetit imesema kuwa Yanga imemalizana na Twite kufuatia mkataba wake kumalizika na imemruhusu kutafuta timu ya kujiunga nayo katika Dirisha dogo lililofunguliwa. Twite alisajiliwa na Yanga misimu minne iliyopita akitokea APR ya Rwanda na usajili wake uligubikwa na mizengwe kibao hasa wapinzani wao Simba nao walihusika kukamilisha usajili wake ambapo baadaye Yanga nao wakamsajili. Haijajulikana kama Twite ataelekea Msimbazi kwenda kulipa fadhila kwani ilidaiwa alikula fedha zao za usajili kabla ya kuelekea Jangwani

Hamosnota kutambulisha wimbo wake Jumamosi

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Hashim Momba Hamosnota amepanga kuutambulisha wimbo wake mpya wa Pole siku ya Jumamosi ijayo katika kituo kimoja cha redio. Akizungumza na Mambo Uwanjani, amesema ameamua kuachia wimbo huo redioni ili kuwafikia mashabiki wake, msanii huyo amepanga pia kuutengenezea video wimbo huo Msanii Hamosnota akionyesha Cd yenye wimbo wake Akiwa katika pozi

YANGA WAMWONYESHEA MLANGO WA KUTOKEA MBUYU TWITE, LWANDAMINA AMRUDISHA

Picha
Na Ikram Khamees. Uongozi wa mabingwa wa soka nchini Yanga SC wenyewe wamemtema beki kiraka Mbuyu Twite na wakitangaza kumuandalia mechi ya heshima ili kumstaafisha bila ridhaa yake. Lakini kocha mkuu Mzambia George Lwandamina akasikia na kusema haiwezekani, Lwandamina anataka kuona uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja ili akiamua wa kumtema anamtema kwa haki. Kwa maana beki huyo amerejea kwenye kikosi cha Yanga kuangaliwa upya na kama kocha huyo hatoridhika naye anaweza kumtema, Obrey Chirwa ndiye anatupiwa macho kutemwa kwavile Yanga ina washambuliaji wengi kuliko mabeki

Mwamuzi wa Ligi Kuu Bara asema yeye ni Yanga damu

Picha
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam Mwamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Maulid Mwikalo amesema kwamba yeye aliwahi kuwa shabiki wa damu wa Yanga SC wakati ule hajaanza kuwa mwamuzi. Hayo aliyasema wakati alipokuwa akihojiwa na mtangazaji mmoja wa kituo cha redio cha jijini Dar es Salaam, Mtangazaji huyo alimuuliza swali mwamuzi huyo kuwa kwa sasa ni shabiki wa timu gani, mwamuzi huyo aliweka wazi kuwa kwa sasa yeye ni shabiki wa Liverpool ya Uingereza. Baadaye alipigwa swali lingine kwamba huko nyuma kabla hujaanza kuwa mwamuzi ulikuwa shabiki wa timu gani, ndipo alipodai kuwa yeye alikuwa Yanga damu tena lialia, mwamuzi huyo amechaguliwa kuwa mjumbe wa chama cha waamuzi mkoani Tabora

Zulu asaini miaka miwili Yanga, aomba subira

Picha
Na Prince Hoza Kiungo wa zamani wa Zesco United, Justine Zulu leo ameanguka saini ya miaka miwili kukipiga na mabingwa wa soka nchini Yanga SC utakaomfanya atumikie kikosi hicho hadi mwaka 2018. Zulu aliyewasili nchini juzi amesaini Yanga likiwa ni chaguo la kocha mkuu George Lwandamina ambaye pia alikuwa akiikochi Zesco. Kutua kwa nyota huyo aliyeiwezesha Zesco kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, kunatishia uwepo wa nyota mmoja wa kigeni, Yanga kabla ya ujio wa Zulu, Yanga ilikuwa na nyota saba wa kigeni ambao ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, Obrey Chirwa raia wa Zambia na Amissi Tambwe raia wa Burundi

Soma.ujumbe wa mwisho wa kipa wa Chapecoense

Picha
Golikipa wa Chapecoense Danilo aliyeokolewa kutoka kwenye ajali ya ndege iliyoanguka Medellin, Colombia alifariki baada ya kuvuja na kupoteza damu nyingi sana ndani na pia kuharibika viungo vyake. Inasemekana kabla ya kufariki alisema maneno haya: “Yesu itazame familia yangu kisha chukua uhai wangu haraka. Tayari baadhi ya rafiki zangu wananisubiri mbinguni, wanahitaji golikipa huko walipo.”