Taifa Jang' ombe yaifanyizia Jang' ombe Boys
Na Prince Hoza, Zanzibar
Timu ya Taifa Jang' ombe maarufu Wakombozi wa Ng' ambo usiku wa leo wameibuka na ushindi wa bao 1-0 katika uwanja wa Amaan Zanzibar mchezo wa ufunguzi kombe la Mapinduzi.
Ushindi huo umewapa nguvu Wakombozi hao wa Ng' ambo ambao Jumapili watacheza na Wekundu wa Msimbazi usiku wa saa 2:30 uwanja huo huo wa Amaan.
Michuano hiyo itaendelea tena Jumapili ya January mosi mwaka 2017 ambapo jioni ya saa 10: 00 KVZ na URA zitaumana na kufuatiwa na mchezo mwingine utakaopigwa usiku wa saa 2:30 Simba SC itakapocheza na Taifa Jang' ombe