Azam yafukuza benchi la ufundi

Na Salum Fikiri Jr, Dar es Salaam

Uongozi wa Azam FC umelitimua benchi lake la ufundi hasa kufuatia mwenendo mbaya wa kikosi hicho, Kocha mkuu Mhispania Zeben Hernandez na msaidizi wake Jonas Garcia.

Inadaiwa makocha hao wameshindwa kuiletea mabadiliko timu na ndio kwanza wameshusha morali, Azam haipo kwenye ushindani na miamba Simba na Yanga zinazofukuzana kileleni.

Mpaka sasa Azam inasuasua ikishika nafasi ya tatu huku ikitoka sare mechi mbilj mfululizo na kuzidi kuongeza gepu la pointi na vinara wa Ligi hiyo Simba pamoja na Yanga wanaoshika nafasi ya pili.

Kally Ongala ambaye kwa sasa ni kocha wa Majimaji ya Songea anatajwa kumrithi Mhispania huyo aliyekuja kwa mikwara akidai Paskal Wawa si beki na kuamua kuachana naye pamoja na kiungo Jean-Bapstita Mugilaneza akidai si kiungo

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA