Tambwe ainusuru Yanga kulala mbele ya Lyon
Na Ikram Khamees
Mshambuliaji wa kimataifa wa Yanga SC raia wa Burundi, Amissi Joselyin Tambwe ameinusuru timu yake kulala mbele ya African Lyon katika uwanja wa Uhuru baada ya kufungana mabao 1-1.
Kwa matokeo hayo Yanga imebaki katika nafasi yake ya pili ikiwa na pointi 37 baada ya leo kushindwa kukwea kileleni endapo ingechomoza na ushindi.
Timu hizo zinaenda mapumziko zilikuwa hazijafungana, lakini kipindi cha pili Lyon ilijipatia bao la kuongoza lililofungwa na Ludovic Venance, Amissi Tambwe aliiokoa Yanga baada ya kusawazisha goli na kufanya matokeo kuwa sare