Yadaiwa Cheka alimkwepa Dulah Mbabe

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Inasemekana bondia wa ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka alimkwepa bondia mwenzake Abdallah Pazi maarufu Dulah Mbabe ambaye ilikuwa apambane naye Desemba 25 wakati wa sikukuu ya Krismasi.

Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa Cheka ambaye amekataa kutaja jina lake, amesema Cheka amemkimbia Dulah Mbabe kwani kwa sasa uwezo wake wa kupigana umeshuka hivyo kama angezichapa naye huenda angepigwa vibaya.

Rafiki huyo amedai Cheka tangia alipopigwa na bondia wa India Vijenger Singh, amepoteza mwelekeo na angejikuta anapigwa vibaya na Dulah Mbabe, "Cheka angepigwa na Dulah, suala la kulipwa na promota halina ukweli ni visingizo tu kwani angeumbuliwa vibaya na ngumi, kwa sasa Dulah ndiye mfalme wa masumbwi ukweli ndio huo" amesema rafiki huyo wa Cheka

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA