Jerry Muro aibuka na kuiomba radhi TFF

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Msemaji wa Yanga SC, aliyekifungoni Jerry Muro ameibuka na kuiomba radhi TFF ili imwachie huru na aendelee na majukumu yake ya usemaji ndani ya Klabu hiyo inayokamata nafasi ya pili.

Muro amesema bila yeye Yanga inapwaya kwani hadi sasa Simba inaongoza Ligi hiyo ikiwa imeiacha Yanga kwa tofauti ya pointi 4 na mtani wake Yanga.

Jerry Muro alifungiwa na TFF kutokana na kutoa lugha chafu na kebehi kwa Shirikisho hilo la mpira wa miguu hapa nchini, lakini Muro ameliangukia Shirikisho hilo na kuliomba radhi na kudai kama atasamehewa basi ndio utakuwa mwisho wa Simba kuchonga

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA