Siri zavuja Ajibu kutimkia Misri
Na Saida Salum, Dar es Salaam
Siri zimevuja baada ya mshambuliaji Ibrahim Ajibu kutimkia nchini Misri kufanya majaribio katika Klabu ya Al Haras Hadood inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Udukuzi uliofanywa na Mambo Uwanjani umebaini kuwa mshambuliaji huyo mwenye mabao matatu ameenda kufanya majaribio katika timu hiyo ili acheze soka la kulipwa baada ya kuona uwezo wa kupata namba katika kikosi cha kwanza haupo.
Ajibu alikuwa akiwekwa benchi jambo lililopelekea aombe ruhusa ya kwenda kufanya majaribio, uongozi wa Simba umemruhusu na tayari mchezaji Hugo ameshaondoka nchini