Simba siyo Yanga, yaichapa JKT Ruvu 1-0 na kuzidi kupaa kileleni

Na Prince Hoza, Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu Bara, Simba SC jioni ya leo imezidi kujichimbia kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Ruvu katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliofanyika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

JKT Ruvu ilicheza kandanda safi muda wote na kuonekana kuizuia Simba isipate bao katika kipindi cha kwanza lakini walishindwa kufanya hivyo kwani Shiza Ramadhan Kichuya aliweza kuifungia Simba bao la ushindi.

Kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 41 na kuzidi kuziacha kwa mbali Yanga na Azam ambazo ziko katika nafasi ya pili na ya tatu, Simba sasa itacheza na Ruvu Shooting kabla haijaelekea Zanzibar kushiriki Mapinduzi Cup

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA