Simba haikamatiki kileleni, yaizaba Ruvu Shooting 1-0

Na Ikram Khamees, Dar es Salaam

Simba SC imezidi kuelekea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bars baada ya jioni ya leo kuichapa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani bao 1-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kukaa kileleni kwa tofauti ya pointi nne na mshindani wake mkuu Yanga iliyo katika nafasi ya pili, Simba sasa ina pointi 44 wakati Yanga wana pointi 40.

Bao lililoipa Simba ushindi liliwekwa kimiani na kiungo mshambuliaji Mohamed Ibrahim "Kabae", huo ni mchezo wa mwisho kwa mwaka huu kwani michuano ya kombe la Mapinduzi inatarajia kuanza kesho.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA