Griezman aitosa Man United, sasa kutimkia Marekani
Straika wa Atletico Madrid Antoine Griezman amefunguka kuhusu nia yake ya kutaka kucheza soka Marekani huku kukiwa na tetesi kuwa Manchester United imekusudia kumchukua katika usajili wa majira ya joto (Juni- Juni).
Griezman anasema "Naipenda Marekani, nataka kuwa na tiketi za msimu mzima wa NBA na niwe nakwenda kuangalia kila mechi nikiwa na watoto wangu", amesema mshambuliaji huyo.
"Najiona mwenyewe nikiwa huko, Bado sijajua ni jiji gani nitaishi, aliongeza Griezman ambaye ni mfungaji anayetegemewa katika kikosi cha Atletico Madrid