YANGA KUJIPIMA NA JKU KESHO UHURU
Na Prince Hoza
Kikosi cha Yanga jumamosi tar 10/12/2016 kitakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya JKU toka Zanzibar.
Mchezo utafanyika uwanja wa Uhuru utaanza saa 10 kamili jioni.
Kiingilio cha mchezo huo kitakuwa sh.5000/ kwa mzunguko na 10000/= kwa VIP.
Tiketi za mchezo huu zitakua ni za electroniki kwa kadi za Selcom.
Mchezo huu utatumika kumuaga kiungo Mbuyu Twite.