Simione Zaza akataliwa West Ham

Wakala wa mshambuliaji wa Juventus, Simione Zaza anayekipiga kwa mkopo West Ham, Vincenza Morabito amesema nyota huyo ataondoka West Ham katika dirisha la usajili la January kurejea klabuni kwake Juve.

Zaza alitua West Ham majira ya joto lakini hajafanya la maana kwani katika mechi 10 za timu hiyo alizocheza kwenye Primier na kombe la EFL hajaifungia bao lolote.

"Zaza kwa vyovyote anarudi Juve kwa sababu West Ham hawamtaki kwa sasa", alisema Morabito ambaye ni wakala wa straika huyo anayekumbukwa kwa kuweka mbwembwe nyingi kwenye oenalti kisha akakosa katika Robo fainali ya Euro 2016 dhidi ya Ujerumani hali iliyoigharimu Italia kufungasha virago

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA