Rasmi Yanga yaachana na Mbuyu Twite
Na Mrisho Hassan
Mabingwa wa kandanda Tanzania Bara, Yanga SC, imeachana rasmi na beki wake kiraka Mkongoman Mbuyu Twite ambaye sasa ni mchezaji huru.
Taarifa iliyotolewa na Kaimu katibu mkuu wa Yanga Baraka Deusdetit imesema kuwa Yanga imemalizana na Twite kufuatia mkataba wake kumalizika na imemruhusu kutafuta timu ya kujiunga nayo katika Dirisha dogo lililofunguliwa.
Twite alisajiliwa na Yanga misimu minne iliyopita akitokea APR ya Rwanda na usajili wake uligubikwa na mizengwe kibao hasa wapinzani wao Simba nao walihusika kukamilisha usajili wake ambapo baadaye Yanga nao wakamsajili.
Haijajulikana kama Twite ataelekea Msimbazi kwenda kulipa fadhila kwani ilidaiwa alikula fedha zao za usajili kabla ya kuelekea Jangwani