Mwamuzi wa Ligi Kuu Bara asema yeye ni Yanga damu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mwamuzi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Maulid Mwikalo amesema kwamba yeye aliwahi kuwa shabiki wa damu wa Yanga SC wakati ule hajaanza kuwa mwamuzi.

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akihojiwa na mtangazaji mmoja wa kituo cha redio cha jijini Dar es Salaam, Mtangazaji huyo alimuuliza swali mwamuzi huyo kuwa kwa sasa ni shabiki wa timu gani, mwamuzi huyo aliweka wazi kuwa kwa sasa yeye ni shabiki wa Liverpool ya Uingereza.

Baadaye alipigwa swali lingine kwamba huko nyuma kabla hujaanza kuwa mwamuzi ulikuwa shabiki wa timu gani, ndipo alipodai kuwa yeye alikuwa Yanga damu tena lialia, mwamuzi huyo amechaguliwa kuwa mjumbe wa chama cha waamuzi mkoani Tabora

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA