Zulu asaini miaka miwili Yanga, aomba subira
Na Prince Hoza
Kiungo wa zamani wa Zesco United, Justine Zulu leo ameanguka saini ya miaka miwili kukipiga na mabingwa wa soka nchini Yanga SC utakaomfanya atumikie kikosi hicho hadi mwaka 2018.
Zulu aliyewasili nchini juzi amesaini Yanga likiwa ni chaguo la kocha mkuu George Lwandamina ambaye pia alikuwa akiikochi Zesco.
Kutua kwa nyota huyo aliyeiwezesha Zesco kufika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, kunatishia uwepo wa nyota mmoja wa kigeni, Yanga kabla ya ujio wa Zulu, Yanga ilikuwa na nyota saba wa kigeni ambao ni Mbuyu Twite, Haruna Niyonzima raia wa Rwanda, Thabani Kamusoko, Donald Ngoma raia wa Zimbabwe, Obrey Chirwa raia wa Zambia na Amissi Tambwe raia wa Burundi