Yanga wanatupia tu, waichinja Ndanda 4-0
Na Mrisho Hassan, Dar es Salaam
Mabingwa watetezi Yanga SC jioni ya leo imeichapa bila huruma.Ndanda FC mabao 4-0 uwanja wa Uhuru Dar es Salaam mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mapema kabisa Yanga waliandika bao la kwanza na la pili yote takifungwa na mshambuliaji wake Mzimbabwe Donald Ndombo Ngoma, Mrundi Amissi Joselyin Tambwe akaiandikia Yanga bao la tatu hivyo hadi mapumziko Yanga ilikuwa mbele.
Kipindi cha pilj kilianza kwa kasi lakini Ndanda walionekana kubadilika na kucheza kwa taadhali kubwa ili wasifungwe odadi kubwa ya mabao, Beki Mtogo Vincent Bossou alifunga goli la nne na la ushindi ambalo liliwafanya Yanga wafikishe pointi 40 wakiendelea kushikilia nafasi ya pili nyuma ya Simba inayoongoza Ligi.
Mchezo mwingine Mtibwa Sugar imeifunga Majimaji ya Songea bao 1-0 katika uwanja wa Manungu mjini Morogoro