Nyosso asaini Mbeya Warriors
Na Exipedito Mataruma, Mbeya
Mchezaji wa zamani wa Ashanti United, Simba SC, Coastal Union na Mbeya City, Juma Said Nyoso amesaini mkataba wa mwaka mmoja kujiunga na Mbeya Warriors ya Mbeya inayoshiriki Ligi Daraja la kwanza Tanzania Bara.
Nyoso aliyewahi kufungiwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) kwa miaka miwili akidaiwa kumtomasa makalioni mshambuliaji na nahodha wa Azam FC, John Bocco "Adebayor".
Adhabu ya mchezaji huyo inamalizika msimu huu hivyo Nyoso amesaini kama mchezaji huru, Beki huyo amekuwa akijifua kivyake ili kujiweka fiti zaidi