WENGER AICHEKELEA CARDIFF ISIYO NA KOCHA.
Arsenal wana nafasi ya kuimarisha uongozi wao wa Ligi ya Premier ya Uingereza ikiwa watawachakaza Cardiff City, ambao hawana meneja, kwa mara ya pili katika kipindi kichache wakati shindano hilo litakapo rejea siku ya kuadhimisha Mwaka Mpya. Ligi ya Premier iko katika pilika pilika za mechi ya nne ndani ya siku kumi wakati ambao wachezaji na vilabu vya nchi zingine barani Uropa viko kwenye mapumziko ya sherehe za Krismasi. Huku ligi hiyo ikiwa imefikia kati musimu huu baada ya raundi 19 kusakatwa, Arsenal wanamiliki uongozi na alama 42, ikiwa ni mara ya kwanza kilabu hicho kuanza mwaka kileleni tangu kampeni ya 2007-08.