MESSI, RONALDO NA RIBBERY WAINGIA FAINALI BALLON D'OR
FIFA
imethibitisha orodha ya majina ya wachezaji watatu walioingia Fainali
ya kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia wa mwaka 2013, Ballon d'Or
ambao ni mtetezi Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Franck Ribery.
Messi
ameshinda mfululizo mara nne tuzo zilizopita, lakini safari hii ni
Ronaldo anayepewa nafasi kubwa ya kutwaa mpira wa dhahabu.
Mshindi mtarajiwa: Messi anaweza kupokonywa tuzo hiyo na Ronaldo kutokana na mchezaji huyo Real Madrid kuwa juu hivi sasa
Mshambuliaji
huyo wa Real Madrid, amefunga mabao 32 tayari msimu huu kwa klabu na
timu yake ya taifa, huku Messi kwa sasa yupo nje ya kikosi cha Barcelona
kutokana na maumivu ya nyama.
Mabao
yake matatu aliyofunga peke yake, hat-trick wakati Ureno inaifunga 3-2
Sweden katika mechi maalum ya kufuzu Kombe la Dunia, yameongeza hamasa
za watu kumpendekeza kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya pili katika historia
yake.
Ribery,
aliyeiwezesha Bayern Munich kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya,
alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuishinda kabla ya Ronaldo kufanya mambo
makubwa dhidi ya Sweden na FIFA ikaongeza muda wa kupigia kura
washindani.
Mshindi atatangazwa katika usiku wa hafla maalum ya Ballon d'Or mjini Zurich, Usiwis Januari 13, mwakani.
Wakati
huo huo, FIFA pia imethibitisha orodha ya wachezaji wanaowania kuwamo
katika kikosi cha wachezaji 11 bora wa dunia, FIFPro World XI 2013.
Kuna wachezaji wanne wa England kwenye orodha hiyo ambao ni Leighton Baines, Ashley Cole, Steven Gerrard na Wayne Rooney.
KIKOSI BORA CHA WACHEZAJI 11 WA FIFA...
Makipa:
Gianluigi
Buffon (Italy, Juventus); Iker Casillas (Spain, Real Madrid CF); Petr
Cech (Czech Republic, Chelsea FC); Manuel Neuer (Germany, FC Bayern
München), Víctor Valdes (Spain, FC Barcelona).
Mabeki:
David
Alaba (Austria, FC Bayern München); Jordi Alba (Spain, FC Barcelona);
Dani Alves (Brazil, FC Barcelona); Leighton Baines (England, Everton
FC); Jérôme Boateng (Germany, FC Bayern München);Ashley Cole (England,
Chelsea FC); Dante (Brazil, FC Bayern München); Mats Hummels (Germany,
Borussia Dortmund); Branislav Ivanović (Serbia, Chelsea FC); Vincent
Kompany (Belgium, Manchester City FC); Philipp Lahm (Germany, FC Bayern
München); David Luiz (Brazil, Chelsea FC); Marcelo (Brazil, Real Madrid
CF); Pepe (Portugal, Real Madrid CF); Gerard Piqué (Spain, FC
Barcelona); Sergio Ramos(Spain, Real Madrid CF ); Thiago Silva (Brazil,
Paris St-Germain FC); Raphaël Varane (France, Real Madrid CF); Nemanja
Vidić (Serbia, Manchester United FC); Pablo Zabaleta (Argentina,
Manchester City FC).
Viungo:
Xabi
Alonso (Spain, Real Madrid CF); Gareth Bale (Wales, Tottenham Hotspur
FC/Real Madrid CF);Sergio Busquets (Spain, FC Barcelona); Steven Gerrard
(England, Liverpool FC); Andrés Iniesta (Spain, FC Barcelona); Isco
(Spain, Málaga CF/ Real Madrid CF); Mesut Özil (Germany, Real Madrid
CF/Arsenal FC); Andrea Pirlo (Italy, Juventus); Marco Reus (Germany,
Borussia Dortmund); Franck Ribéry (France, FC Bayern München), Arjen
Robben (Netherlands, FC Bayern München); Bastian Schweinsteiger(Germany,
FC Bayern München); Yaya Touré (Côte d’Ivoire, Manchester City FC);
Arturo Vidal (Chile, Juventus); Xavi (Spain; FC Barcelona).
Washambuliaji:
Sergio
Agüero (Argentina, Manchester City FC); Mario Balotelli (Italy,
Manchester City FC/AC Milan); Edinson Cavani (Uruguay, SSC Napoli/Paris
Saint-Germain FC); Diego Costa (Spain, Club Atlético de Madrid);
Cristiano Ronaldo (Portugal, Real Madrid CF); Didier Drogba (Côte
d’Ivoire, Shanghai Shenhua FC/Galatasaray SK); Radamel Falcao (Colombia,
Club Atlético de Madrid/AS Monaco FC); Zlatan Ibrahimovi (Sweden, Paris
Saint-Germain FC); Robert Lewandowski (Poland, Borussia Dortmund);
Mario Mandžukić (Croatia, FC Bayern München); Lionel Messi (Argentina,
FC Barcelona); Neymar (Brazil, Santos FC/FC Barcelona); Wayne Rooney
(England, Manchester United FC); Luis Suárez (Uruguay, Liverpool FC);
Robin van Persie (Netherlands, Manchester United FC).