JUMA KASEJA AJIONDOA YANGA.
KIPA wa Yanga, Juma Kaseja amesema kukaa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi minne kulichangia kupunguza ufanisi wake uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Simba Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam juzi iliyomalizika kwa Yanga kubugizwa mabao 3-1.
Akizungumza na mwandishi wetu, Kaseja amesema kwamba kukaa kwake benchi kwa kipindi kirefu kumechangia yeye kufanya vibaya na kuruhusu goli mbili za kizembe, Kaseja anasema haikuwa makusudi yeye kufungwa magoli hayo ila uwezo wake ulianza kumpotea.
'Mchezaji yeyote yule duniani akikaa nje miezi minne na zaidi kunaweza kuathli kiwango chake, mimi sikuhujumu mechi ile, kwanza mnakumbuka wenyewe jinsi Simba ilivyochangia kuharibu kiwango changu kwa kunitema na kuniharibia nisipate timu', alisema na kuongeza.
'Nimetemwa timu ya taifa sababu sikuwa na timu, halikuwa lengo langu kuruhusu bao hizo ila uwezo wangu umeanza kupungua, lakini sikati tamaa naweza kurudisha kiwango changu kulingana na mazoezi ya pamoja ninavyofanya', aliongeza Kaseja.
Kaseja alitemwa na klabu yake ya Simba katika usajili wa mwezi Julai mwaka huu na kupelekea kipa huyo mkongwe kuondolewa kwenye timu ya taifa inayonolewa na Kim Poulsen, kutemwa kwa kipa huyo kumechangia kusota nje ya uwanja miezi minne hadi kusajiliwa tena na mabingwa wa soka nchini Yanga.
Jumamosi iliyopita Kaseja alikubali kufungwa kirahisi magoli mawili yaliyopelekea kushushiwa lawama na mashabiki wa Yanga ambapo timu yake ya Yanga ililala magoli 3-1.