HULL CITY SASA KUITWA HULL TIGERS.

Klabu ya Ligi ya Premia Hull City imewasilisha ombi kwa FA ya Uingereza kutaka kubadilisha jina lake hadi Hull Tigers kuanzia msimu ujao, BBC waliripoti Jumatano.

Mmiliki wa klabu hiyo Assem Allam anataka kubadilisha jina klabu hiyo ya umri wa miaka 109 kutoka Yorkshire lakini hatua hiyo imepingwa vikali na mashabiki.

Mfanyabiashara huyo mzaliwa wa Misri tayari alibadilisha jina la kampuni inayomiliki klabu hiyo kutoka Hull City Association Football Club hadi Hull City Tigers mwezi Agosti.

Allam anaamini kwamba nembo ya 'Tigers' “itauza zaidi ulimwenguni”.


Mashabiki sugu wa Hull wameapa kupinga hatua zozote za kubadilisha jina la klabu hiyo na wameunga kundi kwa jina "City Till We Die" (City Hadi Kufa Kwetu).

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA