MBEYA CITY YAMPONZA PRINCE HOZA.
Na Mwandishi Wetu
Majanga yameanza kumpata aliyekuwa mkurugenzi wa promosheni katika kampuni ya Modern Publishers Prince Hoza (Pichani) ambao pia ni watoaji wa gazeti maarufu la michezo la Mwanasoka ambalo linasomwa na wapenzi na mashabiki wa klabu ya Simba maarufu wekundu wa msimbazi.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi kinasema kuwa Hoza ambaye ni kiongozi upande wa promosheni katika kampuni hiyo inayomilikiwa na mdau na mwanachama maarufu wa Simba SC Majuto Mbiligenda, taarifa hizo zinadai kuwa ujumbe alioutuma Hoza katika ukurasa wake wa facebook ndio chanzo kilichopelekea kuondoshwa katika kampuni hiyo na kusimamishwa kazi.
Inaemekana kuwa Hoza aliandika katika ukurasa wake wa facebook kuwa yeye si shabiki wa Simba na ameamua kujiunga na Mbeya City inayotokea mkoani Mbeya, Hoza aliamua kufanya hivyo kutokana na mgogoro unaoendelea kufukuta katika klabu hiyo iliyopelekea kusimamishwa kwa mwenyekiti wa klabu hiyo Alhaj Ismail Aden Rage.
Chanzo kilichosababishwa Hoza afutwe kazi yake ni kuonyesha ushabiki wa waziwazi kwa Mbeya City badala ya Simba ambao ndio wanaomfanya awepo katika kampuni hiyo, Hoza alikuwa mkurugenzi wa promosheni zote ambapo alijipatia umaarufu mkubwa alipoendesha chemsha bongo ya shinda jezi ya Simba ambayo ilipata wafuasi wengi kupitia gazeti la Mwanasoka.
Licha ya kujishughurisha promosheni, Hoza alikuwa mwandishi wa makala katika gazeti hilo ambapo alipata kuvuma na kolamu yake ya Darubini yangu, kwa sasa ameondolewa katika kolamu hiyo huku baadhi ya wasomaji wakihoji kulikoni kusimamishwa kwa mdau huyo mkubwa.
Hata hivyo mwandishi wetu aliamua kuwasiliana na mkurugenzi wa kampuni hiyo Majuto Mbiligenda ili kuthibitisha ukweli ambapo alikiri kuwa wameamua kuachana na Hoza kutokana na mambo mbalimbali ingawa hakutaka kuweka wazi, Naye Hoza alitafutwa ili athibitishe ukweli wenyewe simu yake ya mkononi iliita pasipo kupokelewa.
Lakini Mtandao huu unafahamu kuwa Hoza ameponzwa na ujumbe alioutuma kupitia ukurasa wake wa facebook, hata hivyo jitihada za kumpata zinaendelea ingawa inadaiwa kuwa Hoza yuko safarini nje ya Dar es Salaam.