SIRI YAGUNDULIKA KINACHOMUONDOA MANJI YANGA.

Na Salum Fikiri Jr

HATIMAYE siri imegundulika kwamba kinachomuondoa mwenyekiti wa mabingwa wa soka Tanzania bara Yanga Yusuf Manji kufuatia kauli yake aliyoitoa jana wakati viongozi wa timu hiyo walipokutana na kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuteua wajumbe wengine katika kamati mbalimbali zilizoundwa.

Siri iliyogundulika na kuelezwa Mambo Uwanjani kuwa mwenyekiti huyo atogombea tena Uenyekiti katika uchaguzi ujao na kuwapisha wengine wenye nia ya kutaka kuiongoza Yanga, lakini inasemekana Manji amekimbia kivuli chake huku suala la mheshimiwa Rage na klabu yake ya Simba moja kati ya sababu zinazomuondoa mapema Yanga.

Mbali na hilo msimamo wa baraza la wazee la klabu hiyo linaloongozwa na mzee Ibrahim Akilimali ambalo lilipinga waziwazi ajira ya Mkenya kuwa katibu mkuu wa Yanga pamoja na mtunza fedha ambaye alikuwa Mhindi, wazee hao waliendelea na msimamo wao na kupinga wazo la kuanzishwa kwa kampuni.


Inadaiwa wazee hawakutaka Yanga igeuzwe kampuni kitendo ambacho kilitaka kufufua mgogoro mkubwa kama ule wa mwanzo ambao ulizaa Yanga kampuni na Yanga asili, Hivyo Manji akaona Yanga haitawaliki na ni bora atangaze kujiondoa mapema na kuwapisha wengine kuongoza.

Chanzo chetu cha habari ambacho kipo karibu na watu wa timu hiyo kimesema kuwa maamuzi ya Manji yanatokana na sababu hizo, 'Manji alitaka Yanga iwe kampuni ili yeye aweze kununua hisa nyingi na kuimiliki timu hiyo kama ilivyo kwa timu nyingine kubwa za huko Uingereza ambazo zinaendeshwa na mfanyabishara mmoja tajiri.

Man United inaye Glazzer, wakati Chelsea inaye Abramovich, na Yanga ilitakiwa iwe na Manji, kilisema chanzo hicho, Aidha mwenyekiti huyo wa Yanga amekasirishwa na mambo mengi yanayofanyika klabuni hapo ikiwemo wazee kujifanya wao ndio wasemaji wa klabu badala ya mwenyekiti ambaye ni yeye na afisa habari wao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA