MAN UNITED YAICHAPA SHAKHTAR NA KUMALIZA KILELENI KUNDI A, RONALDO AREJEA NA MOTO WAKE REAL
BAO pekee la Phil Jones dakika ya 67, limeipa ushindi mwembamba nyumbani wa 1-0 Manchester United dhidi ya Shakhtar Donetsk Uwanja wa Old Trafford na kumpa ahueni kocha David Moyes.
Ushindi huo unaipandisha kileleni mwa Kundi A Manchester United, baada ya kumaliza na pointi 14 katika mechi sita ilizocheza.
Bayer Leverkursen inashika nafasi ya pili kwa pointi zake 10, Shakhtar ya tatu kwa pointi zake nane na Real Sociedad imeshika mkia kwa pointi yake moja.
Katika mechi nyingine, mshambuliaji Cristiano Ronaldo amerejea kutoka kwenye maumivu ya nyama na kufunga bao katika ushindi wa 2-0 ugenini dhidi ya FC Copenhagen.
Luka Modric aliifungia la kwanza Real Madird dakika ya 25 pasi ya Isco na Ronaldo akafunga la pili dakika ya 48 pasi ya Mreno mwenzake, Pepe.
Real imemaliza na pointi 16, ikiwazidi pointi tisa Juventus katika nafasi ya pili, wakati Galatasaray ina pointi tano. Mchezo mwingine wa Kundi B kati ya Galatasaray na Juventus umeshindwa kufanyika kutokana na mvua kubwa.
Real Sociedad imefungwa 1-0 nyumbani na Bayer Leverkusen, Benfica imeshinda 2 - 1 dhidi ya PSG, Olympiakos Piraeus imeshinda 3 - 1 dhidi ya Anderlecht, Bayern Munich imefungwa 3-2 na Manchester City na Viktoria Plzen imeshinda 2 - 1 dhidi ya CSKA Moskva.