RONALDO ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA MBELE YA MESSI.

Gwiji Cristiano Ronaldo, ametajwa kama mshindi wa tuzo ya mchezaji wa mwaka wa World Soccer mbele ya mtani wake wa jadi, Lionel Messi na kiungo machachari wa Bayern Munich, Franck Ribery, jarida hilo lilitangaza Alhamisi.

Tuzo hiyo inayoamuliwa na kikao cha wanahabari na wafafanuzi wa mchezo huo kutoka sehemu mbali mbali duniani, lilitambua juhudi zake za kustaajabisha zilizotekelezwa na nyota huyo katika klabu chake Real Madrid pamoja na kuongoza taifa lake Ureno kufuzu Dimba la Dunia la 2014 Brazil.

Mara yake ya mwisho kunyakua ilikuwa ni 2008, mwaka ambao pia alitunukiwa lile la mchezaji bora duniani la Fifa Ballon d' Or ambalo anawania dhidi ya wawili hao wakati huu, mshindi akizinduliwa Januari.


Mwalimu mstaafu, Jupp Heynckes na Bayern Munich, ambao walifagia mataji ya Bundesliga, Pokal Cup na lile la Ligi ya Mabingwa barani Uropa musimu jana, walibeba tuzo za meneja na timu bora ya mwaka.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA