MKOLA MAN AHUSISHWA NA FREEMASON, NEMBO YAMPONZA.
Na Exipedito Mataluma
MWANAMUZIKI wa kizazi kipya anayetokea Hale mkoani Tanga Christopher Mhenga maarufu Mkola Man anatajwa kuwemo katika orodha ya wasanii wanaotajwa kuwemo kwenye imani ya kishetani inayoenea kwa kasi nchini ya 'Freemason' huku ikidaiwa nembo anayotumia ndio imemponza.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari vinasema kuwa msanii huyo kwa sasa ameanza kujipatia umaarufu mkubwa na kupata mialiko kadhaa ndani na nje ya Tanzania kiasi kwamba kinawachanganya wengi, pia kuongezeka kwa mashabiki na kupendwa kwa nyimbo zake ukiwemo huu mpya wa 'Kilevi changu' ni sehemu nyingine inayotajwa kuwemo katika imani hiyo.
Pia chanzp chetu kimefichua siri ya msanii huyo kuwa anatumia nembo maarufu ya '5LAMABAD' ambayo ni moja kati ya alama za imani hiyo, kitu kingine kilichoibua tetesi za msanii huyo kujihusisha na freemason ni pale alipopiga picha akifanya tambiko kwenye makaburi ambapo inasemekana watu wenye imani hiyo hupendelea kufanya hivyo.
Baadhi ya wakazi wa Tanga ambao wanamfahamu msanii huyo anayetajwa kutikisa jiji hilo kwa sasa na kuwapiga kumbo wakongwe kadhaa waliokuwa wakitamba katika jiji hilo kama Seif Shaaban Matonya na Wagosi wa Kaya wanadai kuwa Mkola Man anaponzwa na jina lake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mkazi mmoja wa Tanga (Jina kapuni) amedai katika kitabu tukufu cha Biblia jina la Mkolar Man ni la kishetani na linatumiwa zaidi na watu waharifu kama vile majambazi, wauaji, wacheza kamali na ngono.
Pia jina hilo kwa lugha ya kiswahili ni sawa na mtu mkorofi, gaidi na mhuni wa kutupwa, aidha mwandishi wetu alipata taarifa nyingine ya siri kuwa msanii huyo ni mwanachama wa genge hilo na tayari amewasaidia wasanii mbalimbali hapa nchini kujiingiza katika imani hiyo potofu na inayokemewa na viongozi wa dini mbalimbali nchini.
Aidha Mambo Uwanjani ilimtafuta kwa niia ya simu msanii huyo ili aweze kutoa uthibitisho wake bahati mbaya simu yake ilikuwa haipatikani huku jitihada za kumpata zikiendelea.