DORTMUND, MILAN WACHECHEMEA HADI 16 BORA .

Borussia Dortmund ambao walimaliza wa pili msimu uliopita waliepusha aibu ya kubanduliwa mapema Ligi ya Klabu Bingwa na bao la dakika za lala salama lake Kevin Grosskreutz ambalo liliwafikisha Wajerumani hao hadi kwenye 16 bora Jumatano.

Dortmund, ambao waliilaza Olympique Marseille 2-1, Arsenal na Napoli wote walimaliza wakiwa na alama 12 huku timu hiyo ya Bundesliga ikimaliza ya kwanza Kundi F na Wataliano hao kuibuka wasio na bahati na kutemwa kutokana na mechi za moja kwa moja licha ya ushindi wa 2-0 dhidi ya viongozi hao wa Ligi ya Premia Uingereza.

AC Milan watakuwa ndio wawakilishi pekee wa Italia katika awamu ya muondoano. Galatasaray, Zenit St Petersburg na Schalke 04 walijaza nafasi zilizosalia katika 16 bora na watakuwa kwenye droo ya Jumatatu ambayo itakuwa na wawakilishi wane kutoka Ligi ya Premia na kutoka Bundesliga.

Barcelona, ambao wanatarajiwa kuwa na Lionel Messi anayeuguza jeraha dimba litakaporejelewa Februari, walimaliza awamu ya makundi kwa njia ya kipekee huku straika wa Brazil Neymar akiwafungia mabao matatu, yake ya kwanza katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, na wakacharaza Celtic 6-1 uwanjani Nou Camp.

Jose Mourinhoanaweza kusubiri kwa hamu droo kwani Chelsea walishinda Kundi E baada ya kucharaza Steaua Bucharest 1-0 uwanjani Stamford Bridge.

Napoli, ambao sasa watacheza Europa League, ndio wa pili kuwahi kubanduliwa katika awamu ya pili licha ya kuwa na alama 12 kutoka kwa mechi sita wengine wakiwa Paris St Germain waliobanduliwa 1997-98.

Katika hali tofauti kabisa, Zenit kutoka Urusi ambao walimaliza wa pili katika Kundi G ndio wa kwanza kufuzu kwa awamu ya muondoano wakiwa na alama sita.

Dortmund wanaohangaishwa na majeraha walikuwa wamebakia na dakika chache sana kabla yao kutupwa dimba la ngazi ya pili Ulaya pale Grosskreutz alipoona wavu kwa kombora ambalo lilipinduliwa dakika tatu tu kabla ya mechi kuisha wakicheza dhidi ya wachezaji 10 wa Marseille.

"Ilikuwa ni furaha sana kufunga bao kama hilo. Tulistahili, lilikuwa la kufurahisha sana,” alisema mfungaji bao huyo.

Galatasaray walifikisha kikombo safari ya mabingwa wa Italia Juve kwa ushindi wa 1-0 mjini Istanbul, Wesley Sneijder akifunga bao la ushindi dakika za mwisho kwenye mechi ambayo ilirejelewa Jumatano baada ya kusimamishwa Jumanne kutokana na theluji.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA