MECHI YA KILI STARS, HARAMBEE YAOTA MBAWA, UWANJA WAJAA MAJI SASA KUPIGWA NYAYO STADIUM.
MECHI ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kati ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ iliyopangwa kuanza Saa 7:00 mchana huu Uwanja wa Kenyatta, Machakos, imeahirishwa na sasa itachezwa Saa 12:00 jioni Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), Nicholas Musonye amesema kwamba sababu ya kufikia hatua hiyo ni hali mbaya ya Uwanja wa Kenyatta kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo.
Makocha wa timu zote, Kim Poulsen wa Tanzania Bara na Adel Amrouche wa Kenya wamekagua Uwanja na kujiridhisha haufai kuchezewa, ingawa Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF) alikuwa anashinikiza mechi hiyo ichezwe hapo hapo
.
Lakini pamoja na Musonye kutoa uamuzi huo, Nyamweya amewaamuru wafanyakazi wa Uwanja wachote maji uwanjani aking’ang’aniza mechi ichezwe hapo.